• About
  • Advertise
  • Careers
  • Contact
Monday, December 16, 2019
No Result
View All Result
NEWSLETTER
Swahili Cloud
-18 °c
  • HOME
  • BONGO5
  • MPEKUZIHURU
  • MWANANCHI
  • SWAHILITIMES
  • MICHUZI
  • HOME
  • BONGO5
  • MPEKUZIHURU
  • MWANANCHI
  • SWAHILITIMES
  • MICHUZI
No Result
View All Result
Swahili Cloud
No Result
View All Result

Home Mpekuzi Huru

Waziri Lukuvi Awataka Wakurugenzi Wa Halmashauri Kujitathmini Katika Utoaji Hati Za Ardhi

by InterWolf
December 3, 2019
in Mpekuzi Huru
0
Waziri Lukuvi Awataka Wakurugenzi Wa Halmashauri Kujitathmini Katika Utoaji Hati Za Ardhi
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

Askari JKT Wadaiwa Kuua Raia Kwa Kipigo

Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Watishia Kuandamana Kwenda Bodi Ya Mikopo

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu December 16

Na Munir Shemweta, WANMM IRINGA
Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuanza kujitathmini katika idadi ya hati za ardhi wanazotoa kwa wamiliki wa ardhi kwenye halmashauri zao.


Dinemart Online Grocery Ordering & Delivery

Alisema Wizara yake itaanza kutangaza wilaya itakayoongoza katika Upangaji, Umilikishaji na Utoaji Hati za ardhi kwa wananchi ili kubaini hamashauri ambazo ziko nyuma katika kutoa hati za ardhi kwa wananchi.

Lukuvi alisema hayo jana katika mkutano wake wa kusikiliza na kutatua kero za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kupitia programu ya Funguka kwa Waziri uliyofanyika ukumbi wa Siasa ni Kilimo katika Manispaa ya Iringa,

‘’Mkurugenzi ajione fahari kuwaezesha wananchi kwa kupima na kuwapatia hati, kama Mkurugenzi huwezi kutoa hati miliki hata mia moja basi wewe hufai’’ alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, kumilikisha na kumpatia mwananchi hati ya ardhi ni kumuwezesha kiuchumi kwa kuwa anaweza kuitumia hati kwenye shughuli za kimaendeleo na kusisitiza kuwa wakurugenzi wa halmashauri wahakikishe wanapanga na kuwamilikisha maeneo wananchi.

Aidha, Lukuvi alisema kwa sasa wizara yake imejipanga kuhakikisha inasogeza huduma za ardhi karibu na wananchi kwa kuanzisha ofisi za mikoa zitakazokuwa na watendaji wote wa sekta ya ardhi kama vile Wapimaji, Wathamini, Wataalamu wa Mipango Miji pamoja na Wasajili.

‘’Sasa Wapimaji, Wathamini na Wapangaji watakuja hapa Iringa, muundo unaanza mwezi ujao lengo ni kuwapunguzia usumbufu wananchi katika kupata huduma za ardhi’’ alisema Lukuvi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, katika kuboresha huduma za sekta ya ardhi, Wizara yake itatumia mifumo unganishi itakayorahisisha utendaji kazi kwa wataalamu wa sekta ya ardhi ambapo kazi kubwa itakuwa ikifanyika kielektroniki badala ya kutumia makaratasi aliyoaeleza kuwa wakati mwingine husababisha tamaa kwa maafisa ardhi.

Alitolea mfano mkoa wa Dar es Salaama kuwa, ushaanza kutumia mfumo unganishi ambapo sasa wamiliki wa ardhi katika mkoa huo wanapatiwa hati za kielectroniki na kubainisha kuwa lengo la kuwa na mfumo unganishi ni kuondoa urasimu na kurahisisha utendaji kazi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi alieleza kuwa mkoa wake umejitahidi kupunguza kero na migogoro ya ardhi iliyokuwepo miaka ya nyuma kwa kuanzisha utaratibu wa kuwafuata wananchi kwenye maeneo yao kupitia programu ya Iringa Mpya.

Alimueleza Waziri Lukuvi kuwa, kama angekuja mwaka mmoja na nusu uliopita basi ukumbi aliofanyia mkutano wa Funguka kwa Waziri ungekuwa umejaa wananchi wenye kero za ardhi lakini jitihada za mkoa wake zimesababisha mkutano huo kutokuwa na idadi kubwa ya wananchi wenye migogoro ya ardhi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

‘’Muda mwingi nautumia kwenda kwa wananchi na kazi za ardhi zina changamoto kubwa na njia pekee ya kukabiliana nazo ni kutenda haki bila kujali uwezo, kabila ama dini ya mtu’’ alisema Hapi.

Loading…

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
taboola apo chini
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Chanzo


ShareTweetShare

Related Posts

Askari JKT Wadaiwa Kuua Raia Kwa Kipigo

Askari JKT Wadaiwa Kuua Raia Kwa Kipigo

by InterWolf
December 16, 2019
0

Polisi mkoani Rukwa inawashikilia vijana watano wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwanakijiji Sabato...

Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Watishia Kuandamana Kwenda Bodi Ya Mikopo

Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Watishia Kuandamana Kwenda Bodi Ya Mikopo

by InterWolf
December 16, 2019
0

Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) imetoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi...

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu December 16

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu December 16

by InterWolf
December 16, 2019
0

Loading... Advertisement Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi taboola apo...

Watu 37 Walazwa baada ya kula chakula chenye sumu msibani

Watu 37 Walazwa baada ya kula chakula chenye sumu msibani

by InterWolf
December 15, 2019
0

Watu 37 wamelazwa katika hospital ya rufani jijini Dodoma baada ya kusadikiwa wamekula chakula chenye sumu katika msiba uliotokea eneo...

Mwalimu Mkuu Atiwa Mbaroni na TAKUKURU Kwa Rushwa ya Ngono Kwa Mwanafunzi Ili Ampe Cheti

Mwalimu Mkuu Atiwa Mbaroni na TAKUKURU Kwa Rushwa ya Ngono Kwa Mwanafunzi Ili Ampe Cheti

by InterWolf
December 15, 2019
0

TAKUKURU Mkoani Dodoma wanamshikilia Mkuu wa Shule ya Sekondari Serengeti iliyopo Serengeti Mkoani Mara, Baraka Sabi kwa tuhuma za kuomba...

TAHADHARI Kwa Umma Kuhusu Utapeli Msamaha wa Rais

TAHADHARI Kwa Umma Kuhusu Utapeli Msamaha wa Rais

by InterWolf
December 15, 2019
0

Loading... Advertisement Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi taboola apo...

Next Post
Mwili wa dereva taxi Arusha wakutwa umefungwa kamba

Mwili wa dereva taxi Arusha wakutwa umefungwa kamba

JAMII IMETAKIWA KUACHANA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA NA KUGUSHI NYARAKA ZA SERIKALI

JAMII IMETAKIWA KUACHANA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA NA KUGUSHI NYARAKA ZA SERIKALI

Watatu wafa ajalini Mbeya

Watatu wafa ajalini Mbeya

Recommended

LIVE: Rais Magufuli na Rais Museveni Wakifungua Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda

LIVE: Rais Magufuli na Rais Museveni Wakifungua Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda

3 months ago
Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Makamishna wa Tume hiyo

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Makamishna wa Tume hiyo

3 months ago

Popular News

    • About
    • Advertise
    • Careers
    • Contact

    © 2019 All Rights Reserved by GOD

    No Result
    View All Result
    • HOME
    • BONGO5
    • MPEKUZIHURU
    • MWANANCHI
    • SWAHILITIMES
    • MICHUZI

    © 2019 All Rights Reserved by GOD

    Login to your account below

    Forgotten Password? Sign Up

    Fill the forms bellow to register

    All fields are required. Log In

    Retrieve your password

    Please enter your username or email address to reset your password.

    Log In